wana ari ya kushinda mechi hii…tuna nguvu na tunajua namna ya kuwapiga Morocco,”Akaongeza kwa kusema,swala si mchezaji
gani anaanza au washambulizi ni wangapi, bali ni
kazi itakayofanyika uwanjani na ubora wa
wachezaji wa Taifa Stars, Alisema Morocco ni timu kubwa
na ina wachezaji wengi wa kulipwa
lakini inafungika na Taifa Stars itaweka
nguvu kuanzia mwanzo wa mechi.
“Unapocheza mechi kama hii inabidi uweke nguvu
dakika za kwanza za mechi ili umpe mpinzani
wakati mgumu kwa hivyo dakika za mwanzo zitakuwa
muhimu sana katika mechi hii,” alisema.
Poulsen alisema baadhi ya watu nchini Morocco bado
wanaamini kuwa ushindi wa mechi ya awali Jijini
Dar es Salaam wa 3-1 dhidi ya Morocco ulikuw
a wa kibahati tu. “Tunataka kuwadhihirishia kuwa
tunaweza na Taifa Stars sio timu ndogo kama wanayodhani.”
Akizungumzia swala la kuwekewa mazingira
mabaya ya kambi pale wanapocheza mechi za nje,Poulsen
alisema mazingira ya kambi ni mazuri kabisa na
wachezaji wote wako katika hali nzuri na tayari kwa mchezo huu...
“Katika hali ya kawaida ungetegemea hujuma nyingi
ikiwemo hoteli mbovu, viwanja vibovu vya mazoezi na
kadhalika lakini hapa ni tofauti kabisa…kwani
mazingira ni mazuri,” alisema Poulsen.
Taifa Stars imeweka kambi katika Hoteli ya Pullman
iliyoko nje kidogo ya Mji wa Marrakech.
Mungu ibariki Tanzania,Mungu ibariki Taifa stars.