Blogger Widgets
Esto music Tz | Members area : Register | Sign in

[NEWS]: SKILIZA HAPA TAMKO LA SERIKALI KUHUSU KUFUTWA KWA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2012

Friday, May 3, 2013

Share this history on :
Kutoka bungeni leo, hii ni kauli ya serikali kuhusu kuridhia kufutwa kwa matokeo yote ya kidato cha nne 2012 na mitihani hii itasahihishwa upya haraka iwezekanavyo.Taarifa ya tume iliyoundwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuchunguza sababu za kufeli vibaya kwa watahiniwa wa kidato cha nne kwa mwaka jana imesomwa leo bungeni na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi.

Kwa mujibu wa taarifa, Waziri Lukuvi amesema sababu zilizosababisha wanafunzi hao kufeli ni pamoja na upungufu wa waalimu, mazingira magumu ya kufundishia, idadi kubwa ya shule za sekondari iliyopelekea idadi kubwa ya watahiniwa na utaratibu mbovu wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) uliotumika bila kuwashirikisha wadau mbalimbali wa elimu.

Kutokana na mambo haya, matokeo yote ya kidato cha nne 2012 yamefutwa na mitihani itasahihishwa upya
Ungana nasi Facebook Like page yetu hapa chini

Weka Maoni Yako Hapo Chini

Facebook Blogger Plugin by Esto Music Tz