Blogger Widgets
Esto music Tz | Members area : Register | Sign in

[NEWS]MATONYA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA UTAPELI SOMA HAPA

Monday, June 10, 2013

Share this history on :
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhcF9s4PjxZIFQdEOMDBrnJGS4NRp-w-AMhAdUcAAbmdi8Y8vIU70XGpJbJRP68pBeBXYTWXMMDsBzeUaYl9J-kn7Lhyw7Rw9pAu6aciLUKDURk_46EHgE1CVxFTcv8Fyrk2w9sKg7xaP4m/s1600/Matonya.jpgMsanii huyo amekamatiliwa kutokana na kufanya utapeli katika show aliyotakiwa kufanya katika ukumbi wa Jambolee uliyopo manispaa ya Songea mkoani ruvuma. Baada ya kuja ukumbini akiwa amelewa hali iliyompelekea kushindwa kufanya show na kusababisha hasara katika ukumbi baada ya kufanya fujo ya kuvunja vitu ukumbi hapo, Ndipo waandaaji wa show hiyo walipo amua ifanyike kesho yake na kiingilo kiwe ni  kununua bia .

Wakati huo msanii huyo alitakiwa akafanye show ingine wilaya ya Mbinga ambayo ilikuwa ni sehemu ya mkataba wao lakini hakufanya hivo na matokeo yake akaamua kukata Tiketi kurudi Dar es Salaam , Baada ya kuvuja taarifa hizo walimfata hadi alipo kuwa amefikia nakukuta amehamia sehemu ingine. 
Hatua iliyochukuliwa nikumvizia katika bus ndipo alipokamatwa , Hadi sasa yupo mahakama ya mwanzo , Taarifa zaidi zinakuijia endelea kufatilia katika mtandao wetu zitakuhijia kwani mwandishi wetu yupo eneo la tukio ,
Endelea kutembelea blog hii tutakujuza zaidi
Ungana nasi Facebook Like page yetu hapa chini

Weka Maoni Yako Hapo Chini

Facebook Blogger Plugin by Esto Music Tz