Blogger Widgets
Esto music Tz | Members area : Register | Sign in

[NEWS]"KAMA NINGEKUA RUGE NINGEMPIGIA MAGOTI LADY JAYDEE NA KUMUOMBA MSAMAHA" ALISEMA SEBO WA MAGIC FM

Tuesday, June 11, 2013

Share this history on :
Katika kipindi cha Sun Downer cha Magic FM, mtangazaji huyo amesema kwamba shangwe zilizolipuka mara baada ya Jaydee kutajwa kuwa miongoni mwa wanaowania tuzo ya msanii bora wa kike katika  tuzo za KTMA, ni ishara ya mwanadada huyo kukubalika katika  jamii.

Mtangazaji huyo amesema kwamba Jaydee ni mwanamke mwenye uthubutu katika  harakati za kuyasaka maisha na kwamba yeyote mwenye nia ya kukwamisha jitihada zake aibu na iwe juu yake. 

Ameongeza kuwa kukubalika kwa mwanadada huyu pia kulidhihirika pale  watazamaji katika tukio hilo walipomshinikiza Meneja wa msanii huyo (Gadna) kutaja kiingilio na tarehe ya maadhimisho ya miaka 13 ya Jaydee 

Hivyo, Sebo anaona ni vyema Ruge akajishusha na kumaliza tofauti zake dhidi ya Jaydee.
Ungana nasi Facebook Like page yetu hapa chini

Weka Maoni Yako Hapo Chini

Facebook Blogger Plugin by Esto Music Tz